Hali maada
Kutoka Wikipedia
Hali ya maada ni muundo jinsi maada hutokea katika hali mbalimbali, ama kama elementi (dutu tupu) au kama kampaundi (dutu za mchanganyiko). Duniani kwa kawaida kuna hali tatu ya mada:
- Hali ya nne ni utegili (plasma) lakini duniani inatokea tu katika maabara penye joto, baridi au shindikizo kubwa sana. Lakini katika ulimwengu kwa jumla maada nyingi iko katika hali ya utegili kwa sababu atomi za jua na maada ya nyota ziko katika hali ya utegili kutokana na joto kali na shindikizo kubwa.
Hali za maada hutofautiana jinsi vipande vidogo ndani ya dutu yaani atomi au molekuli zake zahusuiana.
Katika hali mango zakaa pamoja kila atomi mahali pake. Tunasema: Dutu ni imara. Dutu katika hali hii ina umbo, mjao na uzani maalumu.
Katika hali kiowevu atomi zina nafasi ya kuachana na kubadilishana mahali. Twasema dutu ni kama majimaji. Dutu katika hali hii ina mjao na uzani maalumu lakini haina umbo. Kiowevu chakubali kila umbo la chombo kinamomwagwa.
Katika hali ya gesi atomi hazishikwi pamoja zaelea kwa mwendo huria. Atomi na molekuli za gesi huelekea kusambaa na kukalia nafasi yote ambamo imewekwa. Dutu katika hali hii ina uzani lakini haina umbo wala mjao kamili.