Atomi
Kutoka Wikipedia
Atomi (pia: atomu; kutoka kigiriki ἄτομος átomos "yasiyogawiwa") ni sehemu ndogo ya maada yenye tabia ya kikemia kama elementi.
Atomi ya haidrojeni, oksijeni au chuma ni sehemu kabisa ya elementi hizi. Lakini atomi yenyewe hufanywa na sehemu ndogo zaidi hasa protoni, neutroni na elektroni. Sehemu hizi ndogo zaidi hazina tabia ya elementi fulani ila tu atomi yote ni elementi.
Yaliyomo |
[hariri] Muundo wa atomi
Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani. Kwa sababu hiyo wataalamu waliunda vielelezo mbalimbali vinavyojaribu kuunganisha tabia mbalimbali za atomi zinazopimiwa.
Kielelezo cha Ernest Rutherford kinasema ya kwamba kwamba katikati ya atomi kuna kiini chenye sehemu kubwa ya mada ya atomi yote. Kiini hufanywa na protoni na neutroni.
Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa mizingo elektroni. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.
[hariri] Chaji na ioni
Protoni zina chaji ya chanja, neutroni hazina chaji na elektroni zina chaji ya hasi. Kiini inafanywa na protoni zenye chaji chanja pamoja na neutroni zisizo na chaji hivyo kiini cha kila atomi kina chaji chanja. Elektroni zenye chaji hasi zazunguka kiini.
Kwa jumla chaji hizo husawazishana na atomi yote ni batili yaani haionyeshi chaji maalumu.
Atomi inaweza kuingia katika hali ya kuwa na chaji kama elektroni moja inaongezwa au kuondolewa katika ganda lake halafu atomi hiyo huitwa "ioni".
Kama idadi ya elektroni imepungua chini ya kiwango cha kawaida atomi yote ina chaji chanja na kuitwa "kationi". Kama elektroni imeongezwa chaji ya atomi yote huwa hasi na kuitwa "anioni".
[hariri] Njia za elektroni
Kufuatana na kielezo cha Niels Bohr kiini huzungukwa na mizingo elektroni mbalimbali kama kitunguu. Idadi ya mizingo hutegemeana na idadi ya elektroni au ukubwa wa atomi kwa jumla.
Ukubwa wa atomi yote hutegemeana na umbali wa mzingo elektroni wa nje. Ieleweke ya kwamba mizingo hii yote si dutu au mada lakini nafasi ambako elektroni zazunguka kiini kwa mkasi mkubwa.