Bahari ya Hindi
Kutoka Wikipedia
Bahari ya Hindi ni bahari kubwa ya tatu duniani ikiwa imechukua asilimia 20 ya uso wa dunia. Upande wa kaskazini imepakana na Asia ya Kusini; magharibi imepakana na Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Shamu na Afrika; mashariki imepakana na Ghuba ya Malay, visiwa vya Sunda (Indonesia), na Australia; na kusini imepakana na Bahari ya Kusini.
Bahari hii ni njia muhimu ya usafirishaji na usafiri kwa meli kati ya Asia na Afrika.