Wilhelm Conrad Röntgen
Kutoka Wikipedia
Wilhelm Conrad Röntgen (27 Machi, 1845 – 10 Februari, 1923) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa ugunduaji wa mionzi ya eksirei. Mwaka wa 1901 alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
Elementi sintetiki ya Roentgeni ilipewa jina kwa heshima yake Roentgen.