Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Umaru Yar'Adua - Wikipedia

Umaru Yar'Adua

Kutoka Wikipedia

Umaru Yar'Adua
Umaru Yar'Adua

Umaru Musa Yar'Adua (* 1951, Katsina) ni mwanasiasa wa Nigeria na rais wa nchi tangu 2007.

Yaliyomo

[hariri] Familia yake

Yar'Adua ni Mwislamu aliyezaliwa katika familia ya Wafulbe katika Nigeria ya Kaskazini. Babake Musa Yar'Adua alikuwa waziri katika serikali ya kwanza ya nchi baada ya uhuru. Kakaye jenerali Shehu Musa Yar'Adua alikuwa makamu wa rais chini ya Olusegun Obasanjo kati ya 1976 hadi 1979 akafungwa jela chini ya udikteta wa Sani Abacha.

[hariri] Elimu yake

Umaru Yar'Adua alisoma kemia tangu 1972 kwenye chuo kikuu cha Ahmadu Bello mjini Zaria akawa mwalimu kwenye vyuo mbalimbali. Tangu 1983 akaacha mafundisho akijishughulisha na makampuni mbalimbali.

[hariri] Gavana

1999 baada ya serikali ya Abacha alichaguliwa kuwa gavana wa jimbo la Katsina akarudishwa mwaka 2003.

[hariri] Mwanasiasa asiye na rushwa?

Yar'Adua alisifiwa kwa sababu alitangaza mali yake kabla ya uchaguzi 1999 und 2003. Anasemekana alikuwa gavana aliyekataa rushwa. Aliykuwa kati ya magavana wachache wasiochunguliwa na mamlaka ya kupambana na rushwa "Economic and Financial Crimes Commission".

[hariri] Gavana na shari'a

Alipingwa kwa sababu alishiriki katika tangazo la muundo wa shari'a ya Kiislamu kuwa sheria ya jimbo wakati yeye ni gavana; Katsina ilikuwa jimbo la tano katika Nigeria iliyotangaza shari'a. Pia kesi ya mama Amina Lawal ilitokea chini ya ugavana wake. Mama huyu alishtakiwa chini ya shari'a kuwa alimzaa mtoto ilhali hakuolewa akahukumiwa auawe kwa kupigwa na mawe. Baada ya watu wengi kote duniani kuleta maombi na serikali ya kitaifa kupinga hukumu mahakama ya juu ilifuta hukumu na kumwokoa Amina. Yar'Adua anasemekana hakujaribu kumtetea wala kuzuia hukumu ya mauti.

[hariri] Uchaguzi wa rais

Mwezi wa Desemba 2006 Umaru Yar'Adua aliteuliwa kuwa mgombea wa chama cha PDP kwa uchaguzi wa Aprili 2007. Rais Olusegun Obasanjo alimfanyia kempeni akapata kura nyingi na kumchagua kama makamu wake Goodluck Jonathan (gavana wa Bayelsa katika kusini ya Nigeria).

Kura ya 21. Aprili ilipingwa na watazamaji wengi wa kitaifa na kimataifa kwa sababu ya udanganyifu ulioonekana mahala pengi. Hata hivyo Yar'Asdua alitangazwa kuwa mshindi aliyepata asilimia 70 za kura zote.

Wapinzani walidai uchaguzi urudiwe lakini Yar'Adua alikataa akiwakaribisha vyama vyote kuingia katika serikali ya umoja wa kitaifa na kusahihisha sheria ya uchaguzi.

Tar. 29 Mei 2007 akaapishwa kuwa rais mpya wa Nigeria. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi ya kuwa maraisi wawili waliochaguliwa wamefuatana bila kungilia kwa jeshi.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -