Titicaca (ziwa)
Kutoka Wikipedia
Ziwa Titicaca iko kwenye Altiplano ya Andes kati ya Peru na Bolivia.
Ni ziwa kubwa la pili katika Amerika Kusini lenye eneo la kilomita za mraba 8,372. Liko kwa kimo cha mita 3,809 juu ya UB. Maji yake ina kina cha 105 m. Hivyo ni ziwa la juu duniani penye usafiri kwa meli ndogo kuna pia manowari ya jeshi la maji.
Mito 25 inaingia ziwani. Kuna visiwa vingi.