Thomas Mann
Kutoka Wikipedia
Thomas Mann (6 Juni, 1875 – 12 Agosti, 1955) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa riwaya zake, k.m. "Akina Buddenbrook" (kwa Kijerumani Buddenbrooks, iliyotolewa mwaka wa 1900), "Kifo katika mji wa Venice" (Tod in Venedig, 1912), "Mlima wa Ajabu" (Der Zauberberg, 1924) au "Maungamo ya Felix Krull, Tapeli" (Bekenntnisse des Hochstaplers Felix Krull, 1954). Pia aliandika insha nyingi. Mwaka wa 1929 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.