Seoul
Kutoka Wikipedia
Seoul ni mji mkuu na mji mkubwa katika Korea ya Kusini. Kihistoria na hadi 1945 ilikuwa mji mkuu wa Korea yote. Ina wakazi 10,276,968 kwenye eneo la 610 km².
Seoul iko kando la mto Han katikati ya rasi ya Korea karibu na mpaka na Korea ya Kaskazini. Jiji ni kitovu cha siasa, uchumi, utamaduni na elimu ya Korea Kusini.
Seoul ilikuwa mahali pa michezo ya olimpiki ya 1988.