São Paulo
Kutoka Wikipedia
São Paulo (Kireno: Mt. Paulo) ni jiji kubwa la Brazil pia jiji kubwa katika nusudunia ya kusini lenye wakazi zaidi ya milioni 10 jijini au karibu milioni 20 katika rundiko la jiji.
[hariri] Historia
Mwaka 1554 mapadre wawili Manuel da Nóbrega na José de Anchieta walijenga kituo cha misioni pamoja na shule kwa kuwalengea wenyeji asilia wa Brazil.
Kituo kiki kilikuwa mbegu wa kijiji, baadaye mji (1711) halafu jiji la Mt. Paulo.
Wakati wa karne ya 18 kilimo cha sukari kiliimarisha kilimo cha eneo la mji. Karne ya 19 ilileta kilimo cha kahawa na wahamiaji wengi kutoka Ulaya hasa kutoka Italia. Katika karne ya 20 viwanda viliongezeka.
Leo hii jiji ni kitovu cha biashara, huduma na teknolojia cha Brazil yote.
[hariri] Jiografia
São Paulo iko katika nyanda za juu kwenye kimo cha 760 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya kupoa.
Kuna uwanja wa ndege tatu .