Paul Dirac
Kutoka Wikipedia
Paul Adrien Maurice Dirac (8 Agosti, 1902 – 20 Oktoba, 1984) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza sifa za elektroni ndani ya nadharia ya kwanta. Mwaka wa 1933, pamoja na Erwin Schrodinger alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.