Moshi William
Kutoka Wikipedia
TX Moshi William, jina halisi Shaban Ally Mhoja Kishiwa, ni mmoja wa wanamuziki mahiri wa muziki wa dansi nchini Tanzania. Alizaliwa Tanga mwaka 1958 na kufariki dunia Machi 29, 2006 na kuacha mke mmoja na watoto wanne na aliweza kurekodi albamu 13. Kwa miaka mitatu mfululizo, Moshi William alitunukiwa tuzo ya kitaifa ya utunzi bora (2003, 2004, 2005.)
Moshi William alijiunga na bendi kongwe nchini Tanzania OTTU Jazz Band mwaka 1982.