Mauaji ya Halaiki ya My Lai
Kutoka Wikipedia
Mauji ya Halaiki ya My Lai au The My Lai Massacre (tamka: [mi.˧˩˥'lɐːj˧˧], Thảm sát Mỹ Lai, Thảm sát Sơn Mỹ) yalikuwa mauaji ya mamia ya watu waliouawa na kikosi cha majeshi ya Marekani katika kijiji cha My Lai, nchini Vietnam Kusini mnamo tar. 16 Machi, 1968. Katika kumbukumbu za My Lai yameorodheshwa majina ya wahanga wapatao 504.
Yaliyomo |
[hariri] Mauaji ya My Lai
Siku ile kikosi cha wanajeshi wa Marekani chini ya uongozi wa Luteni William Calley walipewa amri ya kutafuta wanamigambo ya Vietkong kijijini wakiambiwa ya kwamba Vietkong walijificha katika eneo lile. Waliambiwa ya kwamba wasingekuta watu raia mle lakini wategemee wanamigambo. Kikosi kilipoingia My Lai hawakuona wanamigambo bali wanawake, watoto na wazee watupu. Wakihofia ya kwamba Vietkong wanajificha kwenye vibanda na nyumba wanejeshi kadhaa walianza kufyatulia risasi kwenye nyumba na mauaji wa kwanza ya wanawake na watoto yalitokea kwa njia hiyo. Baada ya kusikia risasi watu walianza kukimbia kila upande na wanajeshi wengine walipiga risasi kwa wakimbiaji. Baada ya muda kidogo sehemu ya askari waliendelea kuwaua watu wote. Wakapitia nyumba kwa nyumba na kuua wajeruhiwa pia.
Wavietnam 11 waliokolewa na rubani wa helikopta ya Kimarekani aliyeona mauaji kutoka hewani. Alishuka akajaza helikopta na Wavietnam wachache waliobaki akitisha askari wenzake kuwapigia bunduki wakijaribu kuwaua. Rubani aliyeitwa Hugh Thompson alitoa taarifa kwa wakubwa wake.
[hariri] Kufichwa kwa tendo
Taarifa hii pamoja na habari zote zilizohusu mauaji haya zilifichwa ndani ya jeshi. Jenerali mhusika aliagiza taarifa rasmi lakini afisa aliyefanya utafiti aliandika ya kwamba kikosi cha Luteni Calley ilikuwa na mapigano makali huko My Lai kikaua maadui Vietkong 128 na watu raia 22 waliuawa kwa bahati mbaya.
[hariri] Kesi ilifunguliwa
Habari za My Lai zilifichuliwa kwa sababu askari mwingine aliyeungwa baadaye na kikosi cha Calley ingawa hakuwepo My Lai alisikia hadithi nyingi kutoka wenzake na baada ya kuondoka jeshini aliandika barua kwa ofisi ya raisi ya Marekani na wabunge mbalimbali wa Washington alipoeleza habari za My Lai. Mbunge mmoja tu alifuatilia barua akasababisha utafiti rasmi na Luteni Calley pamoja na askari 25 wengine walifunguliwa kesi za jinai ya uuaji.
Tangu Desemba 1969 magazeti ya Marekani yalianza kutuoa taarifa juu ya mauaji ya My Lai. Watu wengi huko nchini na pia duniani kwa jumla walishtuka sana.
Kesi 4 zilifunguliwa mbele ya mahakama ya kijeshi na 1971 Luteni Calley pekee yake alihukumiwa akapewa jela kwa maisha. Lakini rais Nixon aliamua ya kwamba atakaa muda wa jela kwake nyumbani chini ya ulinzi na mwaka 1974 Calley alisamehewa adhabu na rais.
[hariri] Matokeo ya baadaye
Taarifa za My Lai ziliongeza mkasi upinzani dhidi ya vita ya Vietnam ndani ya Marekani.
Leo hii kuna makumbusho mahali pa kijiji cha kale kilichojengwa na shirika la wanajeshi wa zamani wa Marekani.
[hariri] Viungo vya Nje
- An American Tragedy
- The My Lai Courts-Martial 1970
- Into the Dark: The My Lai Massacre
- 1969 TIME article
- 'Blood and fire' of My Lai remembered 30 years later
- My Lai Peace Park Project
- The first public reports by journalist Seymour Hersh about the My Lai Massacre for the St. Louis Post Dispatch, 13 November, 20 November and 25 November 1969.