Lucky Dube
Kutoka Wikipedia
Lucky Philip Dube (3 Agosti, 1964 - 18 Oktoba, 2007) alikuwa mwanamuziki wa Afrika Kusini. Alizaliwa mji wa Ermelo mashariki mwa jiji la Johannesburg. Hasa alipiga muziki wa Reggae. Jina la Lucky alipewa na mama yake mzazi aliyeitwa Sarah, alimpa jina la Lucky akimaanisha amepata bahati kuishi kwani mama yake alikuwa na matatizo ya uzazi hiyvo kupoteza watoto kila alipokuwa mjamzito. Lucky alilelewa na mama yake peke yake bila ya baba yake sababu baba yake alitengana na mama yake kabla ya Lucky kuzaliwa hiyo ilisababisha maisha ya Lucky na mama yake kuwa duni.
Lucky aliuawa na majambazi katika jiji la Johannesburg saa za jioni kwa kupigwa risasi tarehe 18 Oktoba, 2007.
Yaliyomo |
[hariri] Albamu zake
Hapo chini albamu za Lucky Dube zimeorodheshwa kulingana na lugha au mtindo wa muziki.
[hariri] Mbaqanga
- Lengane Ngeyethu (1981)
- Kudala Ngikuncenga (1982)
- Kukuwe (1983)
- Abathakathi (1984)
- Ngikwethembe Na? (1985)
- Umadakeni (1987)
[hariri] Afrikaans
- Help My Krap (1986)
[hariri] Reggae
- Slave (1989)
- Prisoner (1990)
- Together as one (1992)
- House of exile (1992)
- Captured Live (1993)
- Victims (1993)
- Trinity (1995)
- Serious reggae business (1996)
- Taxman (1997)
- The Way It Is (1999)
- Rastas Never Dies (2000)
- Think About The Children (2000)
- The Rough Guide To Lucky Dube (2001)
- Soul Taker (2001)
- The other side (2005)
- Respect (2006)
[hariri] Viungo vya Nje
- Tovuti Rasmi ya Lucky Dube
- Tovuti ya Albamu zote za Lucky Dube
- Habari Kuhusu Mazishi ya Lucky Dube katika Mtandao wa NME.COM