Klaus Barbie
Kutoka Wikipedia
Klaus Barbie (alizawa tar. 25 Oktoba, 1913 – September 25, 1991) alikuwa mwanajeshi wa SS au Schutzstaffel-Hauptsturmführer, na pia alikuwa mmoja wa wanachama wa Gestapo. Alikuwa akifahamika kama the Butcher of Lyon au Mchinjaji wa Lyon.
Yaliyomo |
[hariri] Wasifu
[hariri] Maisha ya awali
Klaus Barbie alizaliwa mjini Bad Godesberg, karibu na mji wa Bonn, Ujerumani. Barbie alizaliwa katika familia ya waumini wa dhebu la Wakatoliki. Wazazi wake wote walikuwwa walimu. Kunako mwaka wa 1923 alipelekwa shule ambayo babake ndiko alikokuwa akifundishia. Baada ya hapo, akapelekwa shule ya bweni ya mjini Trier.
Mnamo mwaka 1925, familia yake ilihamia mjini Trier ambako huko ndiko alikokuwa anasoma. Mnamo mwaka wa 1933, babake na kakake kipenzi Barbie waliiaga dunia. Kifo cha babake kilipeleka bwana mdogo Barbie kuwa mlevi kupindukia na ndipo alipo amua kujiunga na jeshi la vijana la Adolf Hitler, waliliita Hitler Youth.
Mnamo Septemba 1935, alijunga na SD au Sicherheitsdienst (kikosi cha ulinzi), ni tawi maalum la SS. Baadae kidogo alihamishwa kwenda kutumikia nchini Uholanzi. Mnamo mwaka 1942, alihamishiwa mjini Dijon na kunako mwezi Novemba ya mwaka huo huo wa 1942 akahamishiwa mjini Lyon, Ufaransa, ambapo huko ndiko alikokuja kuwa kiongozi wa Gestapo ndogo.
[hariri] Makosa ya kivita
[hariri] Kesi yake ya mauwaji
[hariri] Marejeo
- Makala kuhusu Barbie katika BBC
- http://www.archives.gov/iwg/research-papers/barbie-irr-file.html
- http://www.time.com/time/magazine/1998/int/981109/latin_america.perons_na30a.html
- http://en.wikipedia.org/wiki/Stefano_Delle_Chiaie