Kisiwa cha Pasaka
Kutoka Wikipedia
Kisiwa cha Pasaka (Kipolynesia: Rapa Nui; Kihispania: Isla de Pascua) ni kisiwa cha Chile katika Pasifiki ya mashariki takriban 3,526 km kutoka mwambao wa Chile.
Anwani ya kijiografia ni 27°09′S 109°25′W. Mji mkuu ni waitwa Hanga Roa. Kuna wakazi 3,791.
[hariri] Jiografia
Kisiwa kiko peke yake baharini na visiwa vya karibu ni Pitcairn 2,000 km upande wa magharibi. Kina asili ya kivolkeno. Ni mlima ulioanza kukua chini ya bahari kwenye mgongo mashariki wa Pasifiki 3000 m chini ya UB.
Umbo al kisiwa ni pembetatu lenye urefu mkubwa wa 24 km na upana mkubwa wa 13 km. Eneo lote ni 162.5 km². Mlima mkubwa hufikia kimo cha 509 m juu ya UB.
Kando la kisiwa kikuu kuna visiwa vidogo kadhaa bila watu.
[hariri] Historia
Inaaminiwa ya kwamba kisiwa kilikaliwa na Watu kutoka Austronesia katika milenia ya kwanza BK. Walileta nao ndizi, taro, viazi na miwa pamoja na kuku na panya.
Utamaduni wao ulistawi kwa karne kadhaa na alama zake ni sanamu kubwa za vichwa vya mawe kote kisiwani. Vichwa hivi huitwa "Moai" lakini hakuna uhakika kusudi lao lilikuwa nini. Kuna pia mabaki ya mwandiko uliokuwa mwandiko wa pekee kati ya visiwa vyote vya Polynesia. Inaaminiwa ya kwamba wakati fulani iadi ya wakazi ilifika 10,000 hadi 15,000.
Lakini utamaduni huu uliporomoka kabla ya kufika kwa Wazungu wa kwanza. Wataalamu huamini ya kwamba wenyewji walipata matatizo ya kiekolojia kwa sababu miti yote ilikatwa na rutba ya ardhi ilipotea. Wengine huamini ya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa na athira pia.
Wakati wa kufika kwa Waholanzi waliokuwa Wazungu wa kwanza kukuta kisiwa kile baharini walibaki watu 2,000 - 3,0000 pekee. Kufika huku kulitokea tar. 5 Aprili 1722 ambayo ilkuwa siku ya Pasaka hivyo jina la kisiwa.
Idadi ya wenyeji ikaendelea kushuka kutokana na magonjwa ya nje yaliyokuja na meli zilizopiga hodi kisiwani kila baada ya miaka kadhaa. Katika karen ya 19 watu mamia walikamatwa na Wafanyabiashara wa utumwa.
Chile ilitwaa kisiwa na kukitangaza sehemu ya eneo lake mwaka 1888. Wakati ule kilikuwa na watu 178 pekee. Idadi hii ilikuwa tena. Leo hii takriban theluthi mbili ya wakazi ni Rapanui au wenyeji asilia ya kisiwa. Kwa jumla kuna Warapanui 4,647 (mw. 2002) na nusu yao wanaishi kisiwani na nusu nyingine Chile bara.