Kigali
Kutoka Wikipedia
Kigali ni mji mkuu wa Rwanda pia mji mkubwa nchini.
Iko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali.
Kigali ina wakazi 600,000.
[hariri] Historia
Kigali ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani mwaka 1907 kama kituo cha mwakilishi wa Afrika ya Masharikiy a Kijerumani Richard Kandt. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Wabelgiji ikawa sehemu ya eneo la kukabidhiwa la Ruanda-Urundi chini ya utawala wa Ubelgiji.
Baada ya kugawa kwa Ruanda-Urundi kuwa nchi mbili za Rwanda na Burundi Kgali ikawa mji mkuu wa Rwanda mwaka 1962.
Mauaji ya Watutsi ya mwaka 1994 yalianza Kigali. Mji ulipungukiwa wakazi 100,000 wakati ule.
[hariri] Uchumi
Misingi ya uchumi ya Kigali ni biashara ya kahawa, mifugo na stani.
[hariri] Mawasiliano
Kigali ina kiwanja ccha kimataifa cha ndege. Kuna barabara kwenda Burundi na Uganda. Bildung