Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu
Kutoka Wikipedia
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ni shirika la kimataifa ambalo ofisi yake kuu iko Geneva, Uswisi. Kamati ilianzishwa na Henri Dunant chini ya jina Kamati ya Watano tarehe 9 Februari, 1863. Shabaha zake hasa ni kuwasaidia na kuwalinda watu wakati wa vita. Kamati imezawadiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mara tatu: miaka ya 1917, 1944, na 1963.
Siku hizi, kamati ni mwanachama wa Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu.