Kalisi
Kutoka Wikipedia
Kalisi |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Kalisi |
Alama | Ca |
Namba atomia | 20 |
Mfululizo safu | metali ya udongo alikalini |
Uzani atomia | 40.078 |
Densiti | 1.55 |
Kiwango cha kuyeyuka | 1115 K (842 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 1757 K (1484°C) |
Asilimia za ganda la dunia | 3.39 % |
Hali maada | mango |
Kalisi ni elementi na metali ya udongo alikalini yenye namba atomia 20 kwenye mfumo radidia ina uzani atomia 40.078. Alama yake ni Ca. Jina lahusiana na neno la kilatini calx (mawe ya chokaa).
[hariri] Tabia
Kalisi ni kati ya elementi zinazopatiikana kwa wingi duniani ikiwa na nafasi ya tano na asilimia 3.39 za ganda la dunia ni kalisi. Ikisafishwa hutokea kama metali laini yenye rangi ya nyeupe-fedha.
Inamenyuka rahisi kikemia hivyo haitokei kama elementi tupu lakini kwa kampaundi mbalimbali hasa katika mawe.
Unga wa kalisi au vipande vidogo vya metali huungua moto yenye rangi ya njano-nyekundu, unga hata bila kuwashwa kwa kumenyuka hewani tu.
Kalisi ni muhimu kwa miili ya wanadamu na wanyama pia kwa mimea kwa sababu inajenga mifupa na meno. Ina pia kazi katika mishipa.
[hariri] Matumizi
Kalisi ni muhimu sana katika maisha ya jamii ya kibinadamu. Ujenzi hutegemea sana kalisi na kampaundi zake. Mawe ya chokaa yaliwahi kutumiwa kwa ujenzi wa nyumba tangu miaka maelfu.
Kampaundi za kalisi ni pia msingi wa saruji na hivyo wa ujenzi wa kisasa. Chokaa ni kiungo cha lazima wakati wa kutengeneza feleji.
Salfati ya kalisi (Ca[SO4] • 2 H2O) ni jasi.
Makala hiyo kuhusu "Kalisi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kalisi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |