Henrik Dam
Kutoka Wikipedia
Carl Peter Henrik Dam (21 Februari, 1895 – 17 Aprili, 1976) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Denmark. Hasa anajulikana kwa kugundua vitamini K. Mwaka wa 1943, pamoja na Edward Doisy alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.