Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Frankfurt am Main - Wikipedia

Frankfurt am Main

Kutoka Wikipedia

Nembo Ramani
Bendera ya Mji wa Frankfurt
Mahali pa mji wa Frankfurt katika Ujerumani
Mahali pa mji wa Frankfurt katika Ujerumani
Mkoa: Frankfurt
Jimbo: Hesse
Eneo: 248,13 km²
Wakazi: 659.000 (2006)
Wakazi / km²: 2.659
Urefu juu ya UB: 104 m
Tovuti rasmi: http://www.frankfurt.de/
Politik
Meya Petra Roth

Frankfurt am Main ni kati ya miji mikubwa ya Ujerumani. Ina wakazi 650,000. Rundiko la mji wa Frankfurt pamoja na miji mingine kama Mainz na Wiesbaden inaitwa eneo la Rhein-Main lenye wakazi milioni nne.

Frankfurt ni kitovu cha uchumi ch Ujerumani hasa makao makuu ya benki kubwa. Uwanja wa Ndege wa Rhein-Main ni mkubwa katika Ujerumani. Barabara kuu na njia kuu za reli za Ujerumani hukutana hapa.

Frankfurt ni makao makuu ya Benki Kuu ya Ulaya na Benki Kuu ya Ujerumani.

Mji umekuwa na tabia ya kimataifa. Takriban kila mkazi wa tatu ana asili yake nje ya Ujerumani.

[hariri] Jiografia

Frankfurt iko kando la mto Main.

[hariri] Historia

Jina lamaanisha "kivuko cha Wafranki" maana yake mji ulianzishwa kama kijiji cha watu wa kabila la Wafranki pale ambako mto Main ulipitika kwa miguu kwa sababu maji hapakuwa na kina kikubwa. Mpito huu ulisababisha mahali kustawi na kukua.

Frankfurt ikawa mji muhimu wa Dola takatifu la Roma. Makaisari walipokea taji na cheo hapa mjini hadi 1806. Katika karne ya 19 Frankfurt ilikuwa makao makuu ya Shirikisho la Ujerumani. Ilikuwa pia makao ya bunge la kwanza lililochaguliwa kwa uchaguzi huru katika Ujerumani mwaka 1848. Ikakua kuwa kitovu muhimu cha biashara na mawasiliano.

Mji uliharibiwa kabisa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kujengwa upya tangu 1945. Katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani tangu 1949 Frankfurt ikawa mji mkuu wa kiuchumi wakati Bonn ilikuwa mji mkuu kisiasa.

[hariri] Viungo vya nje

Daraja la mto Main mjini Frankfurt
Daraja la mto Main mjini Frankfurt
Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Frankfurt am Main" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Frankfurt am Main kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -