Frankfurt
Kutoka Wikipedia
Frankfurt ni jina la miji miwili mikubwa nchini Ujerumani. Kwa kusudi la kuitofautisha mara nyingi hutajwa pamoja na mto iliyoko:
- Frankfurt am Main ni mji mkubwa zaidi kati ya Frankfurt mbili iko kando la mto Main katika magharibi ya Ujerumani.
- Frankfurt an der Oder iko kando la mto Oder kwenye mpaka wa Ujerumani na Poland upande wa mashariki
Frankfurt ni pia jina la vijiji viwili na ilikuwa jina la maeneo ya kihistoria katika Ujerumani.
Kwa umbo la "Frankfort" au "Frankford" jina lapatikana katika Amerika ya Kaskazini. Lataja miji iliyoundwa na wahamiaji kutoka Ujerumani.
Maana asilia ya mto yanataja mambo mawili: "Frank" ni jina la kabila ya Kigermanik ya Kale ya "Wafranki". "furt" (kiing.: "ford") ni sehemu ya kupita mto pasipo maji yenye kina kikubwa.