Edmund Hillary
Kutoka Wikipedia
Edmund Percival Hillary (* 20 Julai 1919 - 11 Januari 2008) alikuwa mpelelezi kutoka New Zealand aliyejulikana hasa kutokana milima mingi aliyopanda. Pamoja na sherpa Tenzing Norgay alikuwa mwanadamu wa kwanza wa kufika kwenye kilele cha Mlima Everest tar. 29 Mei 1953.
Alijifunza kupanda milima tangu utoto kwao New Zealand. Alifanya kazi ya kufuga nyuki iliyomwezesha kutumia miezi ya majira baridi ya New Zealand kwa safari zake duniani.
Hillari alikuwa pia mtu wa kwanza aliyevuka bara la Antaktika kwa trekta.