Chinua Achebe
Kutoka Wikipedia
Chinua Achebe (amezaliwa 16 Novemba, 1930) ni mwandishi kutoka nchi ya Nigeria. Ameandika vitabu vingi vyenye riwaya, mashairi na insha. Hadithi zake zinatumia mitindo ya fasihi simulizi ya lugha yake ya asili, Kiigbo. Hata hivyo ameandika hasa kwa Kiingereza. Baadhi ya maandiko yake ni:
- Mambo Huangamia (1958, kwa Kiingereza "Things Fall Apart")
- Hakuna Starehe Tena (1960, kwa Kiingereza "No Longer At Ease")
- Mshale wa Mungu (1964, kwa Kiingereza "Arrow of God")
- Wasichana Vitani (1973, kwa Kiingereza "Girls at War")
- Shida na Nigeria (1984, kwa Kiingereza "The Trouble with Nigeria")
- Picha ya Afrika (2000, kwa Kijerumani "Ein Bild von Afrika")