Boma la Edinburgh
Kutoka Wikipedia
Boma la Edinburgh ni boma kubwa katikati ya mji mkuu wa Uskoti. Liko kwenye kilima cha mwamba ambako kutoka kwake laonekana vizuri kutoka pande zote.
Boma la kwanza lilijengwa Edinburgh katika karne ya 6 au 7. Jengo la kale linalosimama hadi leo ni kanisa la Mt. Margareta kutoka karne ya 11.
Hazina ya kumbukumbu ya kitaifa ya Uskoti inatunzwa bomani kama vile Jiwe la Scone na taji la Uskoti.