Bertha von Suttner
Kutoka Wikipedia
Bertha Félicie Sophie von Suttner (9 Juni, 1843 – 21 Juni, 1914) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Austria. Hasa aliandika riwaya kwa ajili ya kuhamasisha amani ya kimataifa. Mwaka wa 1905 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.