Archibald Vivian Hill
Kutoka Wikipedia
Archibald Vivian Hill (26 Septemba, 1886 – 3 Juni, 1977) alikuwa mwanafiziolojia kutoka nchi ya Uingereza. Hasa alichunguza nishati ndani ya misuli. Mwaka wa 1922, pamoja na Otto Meyerhof alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.