Alexander Fleming
Kutoka Wikipedia
Alexander Fleming (6 Agosti, 1881 – 11 Machi, 1955) alikuwa daktari kutoka nchi ya Uskoti. Hasa anajulikana kwa kugundua penisilini. Alipewa cheo cha "Sir" mwaka wa 1944. Mwaka wa 1945, pamoja na Ernst Boris Chain na Howard Walter Florey alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.