Fransi
Kutoka Wikipedia
Fransi (Francium) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Fransi (Francium) |
Alama | Fr |
Namba atomia | 87 |
Mfululizo safu | Metali alikali |
Uzani atomia | 223 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 18, 8, 1 |
Densiti | 1.87 |
Kiwango cha kuyeyuka | 300 K (27 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 950K (677 °C) |
Hali maada | mango |
Fransi ni elementi na metali alikali yenye namba atomia 87 kwenye mfumo radidia na uzani atomia 223. Alama yake ni Fr. Fransi ni elementi nururifu sana.
[hariri] Tabia
Fransi ni elementi haba mni kwa sababu ya unururifu wake. Kati ya elementi zote zinazotokea kiasili ni haba kabisa isipokuwa Astatini. Nusumaisha ya isotopi yenye maisha marefu ni dakika 21.8 pekee.
Fransi hapatikani kama elementi ya kudumu lakini hujitokeza mara kwa mara wakati wa mbunguo wa Aktini.
[hariri] Matumizi
Haina matumizi nje ya utafiti wa kisayansi kutokana maisha mafupi na uhaba.
Makala hiyo kuhusu "Fransi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Fransi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |