Visiwa vya Mariana
Kutoka Wikipedia
Visiwa vya Mariana ni funguvisiwa ya Pasifiki ya magharibi takriban katikati ya Papua Guinea Mpya na Japani. Vyahesabiwa kati ya visiwa vya Melanesia.
Kwa jumla ni safu ya visiwa 15 vyenye asili ya kivolkeno kati ya 12 hadi 21N na mnamo 145E.
Vyote ni maeneo ya ng'ambo ya Marekani inayotawala funguvisiwa kama vitengo viwili vya pekee:
- Visiwa vya Mariana ya Kaskazini ambavyo ni idadi kubwa ya visiwa hivi na eneo lenye madaraka ya kujitawala
- Guam ambayo ni kisiwa kikubwa pekee ambacho ni kituo cha kijeshi cha Marekani.