Trebonianus Gallus
Kutoka Wikipedia
Trebonianus Gallus (takriban 206 – Agosti 253) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia Juni 251 hadi kifo chake. Alimfuata Decius. Kwanza alitawala pamoja na mwana wa Decius, Hostilian. Hostilian alipokufa na tauni, Trebonianus alitawala pamoja na mwana wake, Volusianus.