Tofaa
Kutoka Wikipedia
Tofaa (pia: tufaha) ni tunda la mtofaa. Ni kati ya matunda yanayovunwa sana duniani. Maua nyeupe hutoa tunda lenye umbo mviringo na kipenyo cha sentimita 5 - 9.
Asili ya mmae iko Asia. Leo kuna takriban aina 7,500 za matofaa. Mavuno ya kila mwaka hufikia tani milioni 55.
Nchi zinazovuna matofaa hasa ni China, Marekani, Uturuki, Ufaransa, Italia na Uajemi.