Ronald Muwenda Mutebi II
Kutoka Wikipedia
Ronald Muwenda Mutebi II. (* 13 Aprili 1955) ni mfalme au Kabaka wa Buganda nchini Uganda.
Alipokuwa mtoto alikimbia 1966 kwenda Uingereza kwa sababu waziri mkuu Milton Obote alimpindua rais wa Uganda aliyekuwa baba yake Kabaka Mutesa II. Ronald alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Cambridge (Uingereza).
Mwaka 1986 alirudi Uganda. Baada ya kuelewana na serikali ya rais Yoweri Museveni alitawazwa 1993 kama kabaka wa 36 wa Buganda.
1999 alifunga ndoa na Sylvia Luswata Nagginda kwenye kanisa kuu la Namirembe mjini Kampala.