Quito
Kutoka Wikipedia
Quito (tamka: "kito" - Kihisp. "San Francisco de Quito") ni mji mkuu wa Ekuador. Mwaka 2005 ilikuwa na wakazi 1,865,541. Quito ni mji mkubwa wa pili nchini baada ya Guayaquil.
Mji uko 20 km kusini ya mstari wa ikweta katika bonde la milima ya Andes kwenye kimo cha 2850 m juu ya UB.
Kuna kiwanja cha ndega na chuo kikuu pamoja na viwanda.
[hariri] Historia
Quito ilikuwa kati ya miji muhimu ya Dola la Inka kabla ya kufika kwa Wahispania. Wakati wa uvamizi wa Wahispania jenerali Rumiñahui wa jeshi la Inka alichoma mji na kuiharibu kabisa kabla ya Wahispania hawakuiteka.
Quito iliundwa upya na Sebastián de Belalcázar mwaka 1534.
Mwaka 1809 wakati wa ghasia katika sehemu mbalimbali za Amerika Kusini dhidi ya serikali ya mfalme mpya wa Hispania Joseph Bonaparte (mdogo wake Napoleon Bonaparte) kamati ya raia katika Quito ilitangaza uhuru wa eneo lake kutoka Hispania. Utawala wa Hispania ulirudishwa kwa mabavu hadi 1822 wakati Hispania ilishindwa na mapinduzi ya Simon Bolivar na kuundwa kwa jamhuri ya Gran Colombia. Baada ya mwisho wa jamhuri hii sehemu zake ziliachana Quito ikawa mji mkuu wa nchi mpya ya Ekuador.