Port-au-Prince
Kutoka Wikipedia
Port-au-Prince ni mji mkuu wa Haiti mwenye wakazi milioni 2. Iko upande wa magharibi wa kisiwa cha Hispaniola katika hori ya Gonave.
Mji ulianzishwa na Wafaransa mnamo 1749. Tangu 1770 ulikuwa mji mkuu wa koloni ya Ufaransa kiswani badala ya Cap-Haïtien. Baada ya mapinduzi ya Haiti ya 1804 ilikuwa mji mkuu wa Hati huru.
Siku hzi idadi kubwa ya wakazi huishi katika mitaa ya vibanda.