Orodha ya makabila ya Kenya
Kutoka Wikipedia
Hii ni orodha ya makabila ya Kenya inavyotokana na orodha ya Ethnologue ya lugha za Kenya.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Kenya, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Kenya na nchi za jirani. Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Kenya kama wakimbizi kutoka vita katika nchi za jirani. Ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Arabia au Uhindi.
- Waboni (pia huitwa Waaweer)
- Waborana
- Wabukusu
- Waburji
- Wachonyi
- Wachuka
- Wadaasanach
- Wadahalo
- Wadigo
- Waduruma
- Waembu
- Waendo
- Wagikuyu
- Wagiryama
- Wagusii
- Waidakho (pamoja na Waisukha na Watiriki)
- Wakalenjin (pamoja na Wakipsigis, Wanandi, Wakeiyo na Watugen)
- Wakamba
- Wakuria
- Walogooli
- Waluo
- Waluhya (au Waluyia)
- Wamaasai
- Wamalakote (pia huitwa Wailwana)
- Wameru
- Wamwimbi
- Wanyala
- Wanyore
- Waokiek
- Waorma
- Wapokomo wa Chini
- Wapokomo wa Juu
- Wapokoot
- Warendille
- Wasabaot
- Wasagalla
- Wasamburu
- Wasanye
- Wasomali
- Wasuba
- Waswahili
- Wataita
- Watalai (pia huitwa Wamarakwet)
- Wataveta
- Wateso
- Watharaka
- Watugen wa Kaskazini
- Waturkana
- Wayaaku