Opus Dei
Kutoka Wikipedia
Opus Dei (kilatini kwa "kazi ya Mungu") au kwa jina kamilii "Praelatura Sanctae Crucis et Opus Dei" ni shirika la kimataifa ndani ya kanisa Katoliki.
Shabaha yake ni kujenga maisha ya kidini kwenye ngazi ya familia na kuwasiaidia waumini kuwa na maisha ya kulingana na mashariti ya imani ya kikristo kufuatana na mafundisho ya kikatoliki.
Shirika lilianzishwa 1928 na padre Mhispania Josemaría Escrivá (1902-1975) mjini Madrid. Makao makuu yake yako Roma.
Ndani na nje ya kanisa katoliki kuna sifa kwa ajili ya kazi ya kichungaji ya shirika hii lakini pia upinzani dhidi mwelekeo wake unaosema ya kwamba Opus Dei inajaribu kutawala kanisa mioyo na dhana za wafuasi wake na kufundisha aina ya Ukatoliki jinsi ilivyokuwa kabla ya Mtaguso wa Pili ya Vatikano. Mapapa Yohane Paulo II na Benedikto XVI walisifu kazi yake mara nyingi.
Makala hiyo kuhusu "Opus Dei" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Opus Dei kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |