Niobi
Kutoka Wikipedia
Niobi (Niobium) |
|
---|---|
|
|
Jina la Elementi | Niobi (Niobium) |
Alama | Nb |
Namba atomia | 41 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 92.90638 |
Valensi | 2, 8, 18, 12, 1 |
Densiti | 8.57 g/cm³ |
Kiwango cha kuyeyuka | 2750 K (2477 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 5017 K (4744 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 1,8 · 10-3 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo | Jina la kale: Colombium |
Niobi ni elementi haba na metali ya mpito yenye namba atomia 41 katika mfumo radidia. Hutokea ndani ya mitapo na rangi yake ni ya kijivu ikisafishwa.
[hariri] Tabia
Niobi ni metali laini yenye rangi ya kijivu. Tabia zake zafanana sana na Tantali. Niobi tupu inayokaa hewani inapata ganda la oksidi lenye rangi ya kijivu-buluu.
[hariri] Kutokea
Haitokei kama elementi tupu lakini ndani ya mitapo mbalimbali kwa kawaida pamoja na Tantali.
Huchimbwa pale ambako mashapo yamekusanya kiasi kikubwa cha niobi ndani yake kwa mfano Brazil na Kanada. Kuna pia akiba zisizotumiwa bado huko Nigeria, Kongo (Kinshasa) na Urusi. Mwaka 2006 jumla la tani 60,000 ilitengenezwa.
[hariri] Matumizi
Niobi hutuumiwa hasa katika aloi za feleji na metali kadhaa. Aloi hizi huwa ni imara sana.
Makala hiyo kuhusu "Niobi" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Niobi kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |