Ngorongoro
Kutoka Wikipedia
Ngorongoro ("Ngorongoro Conservation Area") ni eneo la kasoko kubwa nchini Tanzania mnamo kilomita 180 kutoka Arusha na pia hifadhi la taifa linalojulikana kote duniani. Eneo hili ni sehemu ya Serengeti.
Kuna jumla la wanyamapori wakubwa takriban 25,000 pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati na simba, fisi, chui .
Ngorongoro imepokelewa katika orodha la urithi wa dunia la UNESCO.