Msese (Scolopacidae)
Kutoka Wikipedia
Msese | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Msese mkia-mweusi
|
||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Wasese hawa ni ndege wa jenasi Limosa na Limnodromus katika familia ya Scolopacidae (kusoma kuhusu wasese wengine tazama Msese (Recurvirostridae)). Ndege hawa wana rangi ya kahawa au kijivu na wakati wa majira ya kuzaa rangi inakuwa nyekundu zaidi. Wana mdomo na miguu mirefu na mdomo ni mnyofu au umepindika juu kidogo. Katika Afrika huonekana kando ya bahari, viziwa au mito ambapo hutafuta chakula kwa kutumia kuingiza mdomo wao katika matope. Hula nyungunyungu, wadudu na lava za wadudu. Hutaga mayai matatu hadi sita ardhini katikati ya manyasi mafupi.
[hariri] Spishi za Afrika (na Ulaya)
- Limosa limosa, Msese Mkia-mweusi (Black-tailed Godwit)
- Limosa lapponica, Msese Mkia-miraba (Bar-tailed Godwit)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Limnodromus griseus (Short-billed Dowitcher)
- Limnodromus scolopaceus (Long-billed Dowitcher)
- Limnodromus semipalmatus (Asiatic Dowitcher)
- Limosa haemastica (Hudsonian Godwit)
- Limosa fedoa (Marbled Godwit)