Metali alikali
Kutoka Wikipedia
Metali alikali ni elementi za kundi la kwanza katika mfumo radidia hasa lithi, natiri, kali, rubidi, caesi na fransi. Hidrojeni ni pia elementi ya kundi la kwanza lakini kwa kawaida haionyeshi tabia za metali alikali.
[hariri] Tabia
Zote ni metali zinazong'aa kwa rangi kifedha-nyeupe zenye elektroni moja tu katika mzingo elektroni wa nje yaani zina valensi moja. Kwa sababu hiyo humenyuka haraka na dutu nyingi hazipatikana kwa umbo safi kiasili. Kama zimesafishwa katika maabara zatunzwa katika angahewa ya gesi adimu au ndani ya mafuta bila kugusana na oksijeni.
Kati ya metali ni laina zakatwa kwa kisu. Densiti husianifu ni kidogo.
[hariri] Uhusiano kati ya uzani atomia na tabia mbalimbali
Tabia mbalimbali hubadilika pamoja na kuongezeka kwa uzani atomia: elketrohasi yapungua, mmemenyuko huongezeka na na viwango vya kucemka au kuyeyuka hupungua.
Metali alikali | Uzani atomia | Kiwango cha kuyeyuka (K) | Kiwango cha kuchemka (K) | Elektrohasi (Pauling) |
Lithi | 6.941 | 453.69 | 1615 | 0.98 |
Natiri | 22.990 | 370.87 | 1156 | 0.93 |
Kali | 39.098 | 336.53 | 1032 | 0.82 |
Rubidi | 85.468 | 312.46 | 961 | 0.82 |
Caesi | 132.905 | 301.59 | 944 | 0.79 |
Fransi | (223) | ? 295 | ? 950 | 0.7 |