Joseph Brodsky
Kutoka Wikipedia
Joseph Aleksandrovich Brodsky (24 Mei, 1940 – 28 Januari, 1996) alikuwa mwandishi na mshairi kutoka nchi ya Urusi. Kuanzia mwaka wa 1972 aliishi nchini Marekani. Mwaka wa 1987 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.