John Locke
Kutoka Wikipedia
John Locke (29 Agosti, 1632 – 28 Oktoba, 1704) alikuwa mwanafalsafa Mwingereza aliyetoa nadharia ya "Mkataba Jamii": mkataba huu unahusisha watawala na watawaliwa ambapo watawaliwa huwapa watawala madaraka ya kuongoza kwa kufuata matakwa ya watawaliwa. Nadharia hii ilisaidia kwa kiwango kikubwa kujengwa kwa taifa la Marekani kutoka katika utawala wa Kifalme uliokuwa chini ya Uingereza.