Jangwa la Namib
Kutoka Wikipedia
Namib ni jangwa kubwa kwenye pwani la kusini-magharibi ya Afrika hasa nchini Namibia. Eneo lake linaanza kusini kwenye mto Olifants wa Afrika Kusini na huelekea hadi kusini ya Angola. Jina la Namib limetokana na lugha ya Wanama lamaanisha "pasio na kitu".
Umbo la Namib ni kanda lenye urefu wa 2000 km na upana wa 100-160 km kuanzia mwambao wa Atlantiki. Jangwa limesababishwa na mkondo wa Benguela unaosukuma maji baridi kutoka Antaktika kuelekea pwani la Afrika. Mkondo huu unazuia mvua kunyesha karibu na mwambao hivyo kuleta hali ya hewa kavu.
Namib haina makazi ya watu isipokuwa miji michache pwani. Miji muhimu ni Swakopmund na Walvis Bay penye bandari kuu ya Namibia. Lüderitz ni mji mdogo tu uliokuwa muhimu zaidi zamani za kuchimba almasi karibu na mji huu.
Sehemu ya kusini ya Namib ni maarufu kwa matuta ya mchanga makubwa yanayofikia kimo cha 300m na urefu hadi 30 km.
[hariri] Viungo vya Nje
- "Namibia's Mobile Sculptures", from Awake! magazine (March 8, 2001)