Cordell Hull
Kutoka Wikipedia
Cordell Hull (2 Oktoba, 1871 – 23 Julai, 1955) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa kutoka nchi ya Marekani. Kuanzia 1933 hadi 1944 alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwaka wa 1945 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel kwa Amani kwa ajili ya kazi yake ya kuanzisha Umoja wa Mataifa.