Web Analytics Made Easy - Statcounter

See also ebooksgratis.com: no banners, no cookies, totally FREE.

CLASSICISTRANIERI HOME PAGE - YOUTUBE CHANNEL
Privacy Policy Cookie Policy Terms and Conditions
Carl Velten - Wikipedia

Carl Velten

Kutoka Wikipedia

Carl Velten (1862–1935) alikuwa mtaalamu wa lugha katika Ujerumani aliyekusanya hadithi na desturi nyingi za Waswahili na kutunga Kamusi ya Kiswahili-Kijerumani kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Velten alizaliwa 4 Septemba, 1862 katika kijiji cha Fluterschen, wilaya ya Altenkirchen kwenye mkoa wa Rhine ya Prussia. 1888-1885 alisoma lugha kwenye vyuo vikuu va Bonn na Tübingen. Baada ya masomo alisafiri kutembelea Ufaransa, Uingereza, Algeria, Tunisia na Misri. Alijiandaa kwa utumishi wa serikali ya Ujerumani katika koloni kwa masomo kwenye chuo cha lugha za mashariki Berlin.

[hariri] Kazi yake katika Afrika ya Mashariki

1893 hadi 1896 alikuwa dragoman au mfasiri wa serikali ya kijerumani ya Afrika ya Mashariki. Katika miaka ile alikusanya fasihi simulizi ya wenyeji kama vile masimulizi, hadithi, mila na desturi nyingi. Aliandika maneno ya wasimulizi wake kwa shorthand. 1896 akarudi Ujerumani kuwa profesa wa Kiswahili kwenye chuo cha lugha za mashariki cha chuo kikuu cha Berlin.

[hariri] Maandiko yake

Sehemu ya vitabu vyake alitoa kwa Kiswahili na Kijerumani vilevile. Hivi ni hasa kuhusu masimulizi, mila na desturi alizokusanya wakati wa kufanya kazi Afrika ya Mashariki.

  • Hadithi na Mazimulizi ya Waswahili - Märchen und Erzählungen der Suaheli (Suahelitext: Band XVIII der Lehrbücher des Oriental. Seminars), Berl. 1898
  • (Sarufi ya Kinyamwezi) Grammatik des Kinyamuesi, der Sprache der Wanyamuesi in Deutsch-Ostafrika nebst Wörterverzeichnis, 1901
  • (Mwongozo kwa kujifunza maandishi ya Kiarabu ya Waswahili) Praktische Anleitung zur Erlernung der arabischen Schrift der Suaheli, Gött. 1901
  • Safari za Wasuaheli, Gött. 1901 / Reiseschilderungen der Suaheli, Gött. 1901
  • Desturi za Wasuaheli na khabari za desturi za sheri'a za Wasuaheli, Gött. 1903; Sitten und Gebräuche der Suaheli nebst Rechtsanschauungen, Gött. 1903
  • (Shairi za Waswahili) Prosa und Poesie der Suaheli, Berl. 1907;
  • (Sarufi ya Kiswahili) Praktische Suaheli-Grammatik nebst einem Deutsch-Suaheli - Wörterverzeichnis, 3. Aufl., Berl. 1910
  • (Kamusi ya Kiswahili-Kijerumani) Suaheli-Wörterbuch, 1. Teil, Suaheli-Deutsch, Berl. 1910
  • (Mwongozo wa Kiswahili kwa ajili ya watumishi wa posta) Suaheli-Sprachführer für Postbeamte, Berl. 1910
  • (Kamusi ndogo ya Kiswahili-Kijerumani na Kijerumani-Kiswahili) Taschenwörterbuch der Suaheli-Sprache, Suaheli-Deutsch und Deutsch-Suaheli, Berl. 1911
  • (Desturi za Waswahili) Gebräuche der Suaheli, 1898
  • (Maelezo juu ya majina ya mahali katika Afrika ya Mashariki) Erklärung einiger ostafrikanischer Ortsnamen, 1898
  • (Lugha ya Wahehe) Die Sprache der Wahehe, Grammatik und Wörterbuch, 1899
  • (Lugha ya Kikami) Kikami, die Sprache der Wakami in Deutsch-Ostafrika, 1900
  • (Majina ambayo Wazungu wanapewa na Waswahili) Die Spitznamen der Europäer bei den Suaheli, 1900;
  • (Vitendawili 100 vya Waswahili) Hundert Suaheli - Rätsel, 1904.

[hariri] Marejeo

Lugha nyingine


aa - ab - af - ak - als - am - an - ang - ar - arc - as - ast - av - ay - az - ba - bar - bat_smg - bcl - be - be_x_old - bg - bh - bi - bm - bn - bo - bpy - br - bs - bug - bxr - ca - cbk_zam - cdo - ce - ceb - ch - cho - chr - chy - co - cr - crh - cs - csb - cu - cv - cy - da - de - diq - dsb - dv - dz - ee - el - eml - en - eo - es - et - eu - ext - fa - ff - fi - fiu_vro - fj - fo - fr - frp - fur - fy - ga - gan - gd - gl - glk - gn - got - gu - gv - ha - hak - haw - he - hi - hif - ho - hr - hsb - ht - hu - hy - hz - ia - id - ie - ig - ii - ik - ilo - io - is - it - iu - ja - jbo - jv - ka - kaa - kab - kg - ki - kj - kk - kl - km - kn - ko - kr - ks - ksh - ku - kv - kw - ky - la - lad - lb - lbe - lg - li - lij - lmo - ln - lo - lt - lv - map_bms - mdf - mg - mh - mi - mk - ml - mn - mo - mr - mt - mus - my - myv - mzn - na - nah - nap - nds - nds_nl - ne - new - ng - nl - nn - no - nov - nrm - nv - ny - oc - om - or - os - pa - pag - pam - pap - pdc - pi - pih - pl - pms - ps - pt - qu - quality - rm - rmy - rn - ro - roa_rup - roa_tara - ru - rw - sa - sah - sc - scn - sco - sd - se - sg - sh - si - simple - sk - sl - sm - sn - so - sr - srn - ss - st - stq - su - sv - sw - szl - ta - te - tet - tg - th - ti - tk - tl - tlh - tn - to - tpi - tr - ts - tt - tum - tw - ty - udm - ug - uk - ur - uz - ve - vec - vi - vls - vo - wa - war - wo - wuu - xal - xh - yi - yo - za - zea - zh - zh_classical - zh_min_nan - zh_yue - zu -