Ben Mottelson
Kutoka Wikipedia
Ben Roy Mottelson (amezaliwa 9 Julai, 1926) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Baadaye alihamia na kuchukua uraia wa Denmark. Hasa alichunguza nadharia ya atomu na kugundua mfumo isopacha (kwa Kiingereza asymmetrical shapes) wa kiini cha atomu. Mwaka wa 1975, pamoja na Aage Bohr na James Rainwater alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.