Baikal (ziwa)
Kutoka Wikipedia
Ziwa la Baikal (Kirusi: Озеро Байкал = Osero Baykal) ni ziwa kubwa katika Siberia kwenye sehemu ya Kiasia ya Urusi. Baikal ni gimba kubwa la maji matamu duniani.
Urefu wake ni 636 km, upana 20-80 km na kina kikubwa ni 1,600 m. Hakuna miji mikubwa kando la ziwa lakini Irkutsk ni 60 km kutoka ziwani.
Ziwa hili lina tabia za pekee. Aina 1600 kati ya aina 2,500 za wanayama na mimea za ziwa zinapatikana hapa tu. Nerpa ya Baikal ni sili ya pekee katika maji matamu; samaki ya Omul hupatikana hapa tu.