Rio de Janeiro
Kutoka Wikipedia
Rio de Janeiro ni jiji kubwa la pili nchini Brazil baada ya São Paulo.
Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi 21 Aprili 1960. Leo ni mji mkuu wa jimbo la shirikisho la Rio de Janeiro. Mwaka 2000 rundiko la jiji lilikuwa na wakazi 5,473,909.
Rio de Janeiro ni jiji la Brazil linalojulikana zaidi kote duniani. Ni kitovu cha utalii na cha utamaduni. Kanivali yake inavuta wageni wengi kila mwaka. Mlima wa Corcovado unabeba Sanamu ya Mwokozi ambayo ni sanamu kubwa ya Yesu yenye kimo cha m 30.
[hariri] Viungo vya Nje
- Picha za Rio de Janeiro na vitongoji vyake
- Tovuti ya "City Hall" yenye takwimu mbalimbali za jiji, habari za Kanivali na sheria za manispaa (kwa Kireno).
- Rio de Janeiro kwenye ukurasa wa Wikitravel kwa Kiingereza