Metali
Kutoka Wikipedia
Metali ni kundi la elementi zenye tabia za pamoja kama vile
- zapitisha umeme kirahisi
- zapitisha joto
- zinang'aa
- ni wayaikaji (zinaweza kubabatizwa kuwa wembamba kama waya au kupinduliwa kabala ya kuvunjika)
Kikemia tabia hizi zote zatokana na muungo metali ya elementi hizi. Kinyume chake simetali kwa kawaida ni kechu kama mangu, hazing'ai na zinahami (hazipitishi umeme).
Idadi kubwa ya elementi katika mfumo radidia huhesabiwa kati ya metali. Kuna pia elementi zinazoonyesha tabia kati ya metali na simetali kama vile metaloidi au nusumetali.
Mifano ya metali ni
[hariri] Historia ya matumizi
Metali zimetumiwa na binadamu kwa vyombo vyao tangu zamani. Mwanzoni watu walitumia mawe tu kwa vifaa vingi. Lakini baadaye walitambua faida ya metali.
Katika Asia na Ulaya shaba ilikuwa metali ya kwanza iliyotumiwa na watu. Baadaye waliiyeyusha na kukoroga pamoja na stani kuwa aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Takriban mnamo 1200 KK watu wa kwanza walianza kutumia chuma. Maarifa haya yalienea katika pande nyingi za dunia.
Katika Afrika watu walianza kutumia moja kwa moja chuma jinsi inavyoonekana kutokana na utafiti wa akiolojia katika Nigeria.
[hariri] Kupatikana kwa metali
Metali zapatikana mara nyingi ndani ya miamba mbalimbali kama mtapo. Kunatokea pia ya kwamba zapatikana kama metali tupu. Lakini njia ya kawaida ni kuvunja mwamba mwenye mtapo ndani yake na kutoa metali kwa njia ya joto au kwa kutumia kemikali.
Mahali pa kuchimba metali huitwa migodi. Mara nyingi ni lazima kuchimba chini ya uso wa ardhi ili kupata mtapo.
[hariri] Aloi za metali
Vitu vingi vya kimetali ni mchanganyiko au aloi za metali pamoja na metali nyingi au pia simetali. Aloi zinazotumiwa zaidi ni: