Mahakama Kuu ya Kimataifa
Kutoka Wikipedia
Mahakama Kuu ya Kimataifa (International Court of Justice kifupi ICJ) ni taasisi kuu ya kisheria ya Umoja wa Mataifa (UM). Madaraka yake yamepangwa katika katiba ya UM na makao makuu yapo Den Haag. Iliundwa mwaka 1945 ikachukua nafasi ya mahakama ya kimataifa ya awali iliyofanya kazi chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa.
Ni tofauti na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.
Yaliyomo |
[hariri] Madaraka
Madaraka ya mahakama hii yanahusu madola pekee ambayo ni wanachama wa UM au yale yaliyokubali mapatano juu ya mahakama kuu ya kimataifa. Mahakama inashughulika kesi kama nchi zote husika zimewahi kukubali kesi isikilizwe mbele yake. Tangu kuundwa 1945 hadi mwaka 2003 ilitoa hukumu 76 pamoja na maoni ya kisheria 24.
Hadi 2008 ni nchi 66 zilizokubali madaraka ya mahakama kwa kila kesi itakayotokea kati ya nchi na nchi. Kesi inayohusu nchi nyingine inafunguliwa kama nchi hizi zinakubali mamlaka ya mahakama hii. Nchi zinaweza kukubali madaraka ya mahakama zikiweka maswali maalumu kando. Kwa mfano Ujerumani ilikubali mamlaka ya mahakama isipokuwa kwa kesi zinazohusu mambo ya kijeshi.
Nchi mbalimbali ziliwahi kukataa maazimio katika kesi zilizoanzishwa tayari:
- Afrika Kusini ilikataa azimio la mwaka 1971 la kujiondoa katika Namibia
- Ufaransa ilikataa 1973 azimio la kusimamisha majaribio na mabomu ya kinyuklia kwenye atolli ya Mururoa katika Pasifiki.
- Moroko ilikataa azimio la kuondoka katika Sahara ya Magharibi iliyokuwa koloni ya Hispania iliyovamia0
- Marekani ilikataa 1984 mamlaka ya mahakama katika kesi iliyohusu mipango ya kijeshi kuhusu Nikaragua
Menginevyo nchi zilizowahi kukubali ziliendelea kuitikia hukumu.
[hariri] Muundo
Mahakama ina majaji 15 wa kudumu wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa UM na Baraza la Usalama la UM kwa pamoja kwa muda wa miaka 9. Theluthi moja ya majaji inachaguliwa kila baada ya miaka mitatu. Nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama huwa na jaji mle kila wakati ni China, Marekani, Ufaransa, Ufalme wa Muungano (Uingereza) na Urusi. Nafasi nyingine huzunguka kati ya nchi wanachama wa UM.
Inawezekana kumwongeza jaji kwa kesi maalumu kama nchi ambayo kesi yake inasikilizwa haina jaji katika mahakama inawezekana kumwongeza jaji anayependekezwa a nchi ile.
[hariri] Majaji mwaka 2007
Mwaka 2007 watu wafuatao walikuwa majaji wa kudumu wa mahakama kuu ya kimataifa:
Jina | Nchi | Nafasi | Alichaguliwa | Mwisho wa kipindi chake |
---|---|---|---|---|
Rosalyn Higgins | Ufalme wa Muungano | Jaji menyekiti | 1995, 2000 | 2009 |
Awn Shawkat Al-Khasawneh | Jordani | Jaji makamu wa mwenyekiti | 2000 | 2009 |
Raymond Ranjeva | Madagaska | Jaji | 1991, 2000 | 2009 |
Shi Jiuyong | China | Jaji | 1994, 2003 | 2012 |
Abdul G. Koroma | Sierra Leone | Jaji | 1994, 2003 | 2012 |
Gonzalo Parra Aranguren | Venezuela | Jaji | 1996, 2000 | 2009 |
Thomas Buergenthal | Marekani | Jaji | 2000, 2006 | 2015 |
Hisashi Owada | Japan | Jaji | 2003 | 2012 |
Bruno Simma | Ujerumani | Jaji | 2003 | 2012 |
Peter Tomka | Slovakia | Jaji | 2003 | 2012 |
Ronny Abraham | Ufaransa | Jaji | 2005 | 2014 |
Sir Kenneth Keith | New Zealand | Jaji | 2006 | 2015 |
Bernardo Sepúlveda Amor | Mexico | Jaji | 2006 | 2015 |
Mohamed Bennouna | Moroko | Jaji | 2006 | 2015 |
Leonid Skotnikov | Urusi | Jaji | 2006 | 2015 |
[hariri] Viungo vya Nje
- International Court of Justice, Official site